Kampuni zajitetea baada ya KEBS kusimamisha uuzaji wa aina 10 za mafuta

  • | KBC Video
    50 views

    Kampuni ya kutengeneza mafuta ya kupikia Pwani Oil imepuzilia mbali madai kwamba bidhaa zake hazijaafikia viwango vilivyowekwa na shirika la kukadiria ubora wa bidhaa KEBS. Kampuni hiyo inayoendesha shughuli zake kutoka kaunti ya Mombasa imesema haijawahi tuhumiwa kuhusiana na viwango vya ubora. Hata hivyo kampuni hiyo imesema imeanzisha mpango wa marekebisho kwenye shehena ya bidhaa yake kuambatana na matakwa ya KEBS. Ijumaa iliyopita shirika la KEBS lilitangaza marufuku ya muda ya uuzaji wa aina 10 za mafuta ya kupikia kwa kutoafikia viwango vya ubora.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #kenyaelection2022 #KenyaDecides2022