Kanisa ambayo marehemu Jenerali Ogolla alisaidia kujenga yatakaswa

  • | Citizen TV
    1,878 views

    Kila aliyemfahamu Jenerali Francis Ogolla alimtaja kama mcha Mungu na mtu aliyependa sana dini. Kifo chake kikiwafungulia wakenya ukurasa wa maisha yake, huku kanisa la kianglikana likimtaja kama mtu aliyeheshimu dini yake na kutoa mfano wa kuigwa. Serfine Achieng Ouma alihudhuria ibada katika kanisa la St Thomas ACK Nduru ambalo jenerali Ogolla alishiriki kulijenga na kutuandalia taarifa ifuatayo..