Kanisa katoliki lapinga marekebisho ya katiba kupitia kura ya maamuzi

  • | K24 Video
    49 views

    Viongozi wa kanisa katoliki nchini wamepinga kufanyika kwa marekebisho ya katiba kupitia kura ya maoni baada ya mazungumzo ya Bomas kukamilika ili kusiwe na hali ya atiati nchini. Nalo baraza la makanisa nchini , NCCK, limetaka muda wa kuiangalia upya mipaka ya maeneo bunge uongezwe miaka miwili zaidi ili kuipatia tume huru ya uchaguzi na mipaka , IEBC, muda wa kutosha kufanya shughuli hiyo kwa makini na kuzuia migogoro. Nayo tume ya maadili na kupambana na ufisadi , EACC imetaka wale wote wanaoandamwa na ufisadi wazuiliwe kuwania nafasi zozote wakati wa uchaguzi