Kanisa Katoliki yafunga hospitali ya misheni ya Kerio Valley

  • | Citizen TV
    1,000 views

    Hospitali ya pekee ya Kerio Valley mission pamoja na kanisa katoliki eneo la Chesongoch kaunti ya Elgeyo Marakwet zimefungwa kutokana na mauaji ya padri wa kanisa hilo Father Allois Bett, wiki iliyopitia. Taarifa kwa vyombo vya habari inasema kuwa, usimamizi wa kanisa hilo umeafikia uamuzi huo kwani hali ya usalama katika eneo hilo ni hatari. Kanisa katoliki limetoa masharti kwa serikali kuimarisha usalama na kuwapokonya wakazi bunduki wanazomiliki kinyume cha sheria kabla ya kurejesha huduma eneo hilo.