Kanisa la karne ya 16 laibuka kutoka chini ya maji baada ya ukame

  • | BBC Swahili
    1,092 views
    Mabaki ya Hekalu la Quechula la karne ya 16 yaliyokuwa yamefunikwa na maji yameibuka tena huko Mexico kufuatia ukame na joto kali. Kanisa hilo lilifunikwa na maji wakati Bwawa la Malpaso lilipojengwa katika miaka ya 1960. Hapo awali wakati maji yanapungua lilionekana kidogo lakini sasa linaonekana lote kabisa. #bbcswahili #mabadilikotabianchi #ukame