Kashfa ya shilingi bilioni 3.7 ya vyandarua vya mbu yazidi kutokota

  • | K24 Video
    17 views

    Kashfa ya shilingi bilioni 3.7 ya vyandarua vya mbu ikiwa inazidi kutokota,mamlaka zinazoshukiwa kuhusika zikiwa pamoja na usimamizi wa mbeleni wa wizara ya afya na kemsa zimeendelea kukana madai hayo dhidi yao. Aliyekuwa katibu mkuu wa idara ya huduma za matibabu Peter Tum akiwa mbele ya kamati ya afya ya seneti, ameeleza kuwa majukumu ya malaria na kifua kikuu yalishughulikiwa na idara ya afya ya umma na taaluma, iliyosimamiwa na daktari Josephine Mburu.