Kasisi asiyesikia atawazwa kanisani Presbyterian, Kayole

  • | KBC Video
    Tawi la Kayole Kusini la kanisa la ki-Presbiteri hapa nchini leo liliandikisha historia kwa kumtawaza mhubiri wa pili mwenye matatizo ya kusikia wa kanisa hilo hapa nchini na katika kanda ya Afrika Mashariki. Kutawazwa kwa George Obonyo kunaonekana kuwa hatua ya kuimarisha ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kanisani, mtindo ambao jamii ya watu wenye matatizo ya kusikia na watu wenye ulemavu wanatumai utaigwa katika makanisa mengine kote nchini. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #ThisIsKBC #News