Kasisi John Pesa akanusha kueneza imani potovu

  • | Citizen TV
    1,241 views

    Kiongozi wa kanisa la Coptic Holy Ghost huko Kisumu John Pesa, sasa amekanusha madai ya kuwazuilia wagonjwa katika kanisa lake, akitaja tuhuma hizo kuwa njama ya kumharibia jina na kuwazuia waumini kuhudhuria kanisa hilo. Akizungumza katika kanisa lake hii leo, Pesa alisisitiza kuwa ni mtu mmoja tu aliyekuwa na maradhi ya akili aliyekuwa kanisani humo na wala sio watu 8 kama iliyoripotiwa na asasi za usalama