Katibu Mkuu wa UN awataka viongozi wa dunia kuungana, akieleza dunia inaelekea inayumba

  • | VOA Swahili
    561 views
    Viongozi wa dunia waliofarakanishwa na vita, mabadiliko ya hali ya hewa na muendelezo wa kukosekana usawa wamekusanyika katika sehemu moja Jumanne kumsikiliza mkuu wa UN akiwataka wachukue hatua ya pamoja kukabiliana na changamoto kubwa za kibinadamu – na kuanza kuwasilisha tathmini yao kuhusu masuala muhimu yaliyoko katika majukwaa ya ulimwengu “Dunia yetu inaelekea kuwa inayumba. Mivutano ya kisiasa ya kieneo inaongezeka. Changamoto za kimataifa zinarudikana. Na inaelekea hatuwezi kuungana pamoja kukabiliana nazo,” Antonio Guterres amewaambia watu wanaoendesha mataifa ya ulimwenguni. Hivi sasa tunaelekea katika dunia iliyogawanyika na hili kwa namna nyingi ni jambo chanya. Inaleta fursa mpya za uadilifu na uwiano wa mahusiano ya kimataifa. #unga #voaunga #unga78 #AntonioGuterres - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.