Katibu wa elimu ya msingi Dkt. Julius Jwan azuru Nakuru

  • | Citizen TV
    207 views

    Wizara ya elimu imefafanua kuwa watahiniwa wa shule sitini na saba za kibinafsi ambazo vifaa vya mitihani havikuchukuliwa katika siku ya kwanza ya mtihani wa gredi ya sita na KCPE hapo jana ,walihamia shule mbadala baada ya shule hizo kufungwa miaka miwili iliyopita. Akizungumza baada ya kufungua makasha ya mtihani katika kaunti ya Nakuru hii leo ,katibu wa elimu ya msingi Dkt.Julius Jwan amesema watahiniwa wa shule hizo walisajiliwa miaka mitatu iliyopita na wizara hiyo sasa itaanza kuweka mpangilio ili kuepuka visa kama hivi siku zijazo. Haya yanajiri baada ya maswali kuibuka kuhusu shule sitini na saba katika kaunti za Bungoma na Uasin Gishu ambazo vifaa vya mitihani havikusambazwa kwao hapo jana.