Katibu wa huduma za magereza Esther Ngero ajiuzulu

  • | KBC Video
    20 views

    Katibu wa huduma za magereza Esther Ngero amejiuzulu. Ngero alijiuzulu wiki moja tu baada ya kuhamishwa kutoka idara ya usimamizi na utoaji huduma katika afisi ya waziri mwenye mamlaka makuu hadi huduma za magereza chini ya wizara ya usalama wa kitaifa. Taarifa kutoka mkuu wa utumishi wa umma imemtaja Ngero kuwa nguzo muhimu kwenye uzinduzi wa mpango wa kuimarisha usimamizi na utoaji huduma za serikali na pamoja na usimamizi wa taasisi za serikali katika wizara mbali mbali Ngero ambaye ni mtaalamu wa uhasibu aliteuliwa kuwa katibu baada ya kuhudumu kwa miongo miwili katika sekta ya mafuta. Rais William Ruto amemshukuru Bi Ngero kwa huduma zake kwa taifa na kumtakia kila la heri maishani.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channell: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #darubini #resign