Kauli ya ACT baada ya Mpina kuenguliwa

  • | BBC Swahili
    46,936 views
    Tanzania inatarajiwa kuandaa uchaguzi Mkuu baadaye mwezi Oktoba. Tume ya kusimamia uchaguzi INEC imepokea na kuidhinisha watakaogombea Urais na Manaibu wao yaani wagombea wenza wao. Rais Samia Suluhu Hassan ameshaidhinishwa kuwania kiti hicho huku INEC ikitarajiwa kuto aorodha kamili ya wagombea Urais wakati wowote kuanzia sasa. Ila hatima ya Luhaga Mpina imejulikana baada ya tume hiyo kumzuia hata kufika ndani ya ofisi zao mapema leo. Je, ana uwezo wa kupinga suala hili mahakamani, ama ndio mwisho wake kwa sasa? @RoncliffeOdit anachambua suala hili kwa mapana na marefu saa tatu usiku wa leo, mubashara kwenye Dira ya Dunia TV kupitia ukurasa wa YouTube wa BBC Swahili Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw