Kaunti ya Kirinyaga yawapa walimu wa chekechea ECDE ajira ya kudumu

  • | Citizen TV
    118 views

    Kaunti ya Kirinyaga imetangaza kuwapa walimu chekechea ECDE ajira ya kudumu yenye pensheni . Kwa mujibu wa gavana wa kaunti hiyo Anne Waiguru, mpango huo utawafaidi walimu 420 ambao wamekuwa wakihudumu chini ya kandarasi kwa miaka mitatu sasa. Akizungumza kwa niaba ya serikali ya kaunti hiyo, waziri wa elimu wa Kirinyaga James Kinyua Mutugi, amesema kuwa mpango huo unaanza mara moja katika mwezi huu. Kinyua alikuwa akihutubia walimu wa chekechea katika chuo cha mafunzo anuwai cha vijana cha Kaitheri.