Kaunti ya Makueni yajiandaa kwa siku ya kitaifa ya kupanda miti

  • | Citizen TV
    540 views

    Matayarisho ya siku ya upanzi wa miti itakayoongozwa na rais Wiliam Ruto jumatatu ijayo yanaendelea katika eneo la Kiu, kaunti ndogo ya Makindu kaunti ya Makueni ambapo waziri wa mazingira Soipan Tuya alisema serikali inapania kupanda miti milioni Mia tano siku hiyo. Viongozi mbalimbali wakiongozwa na katibu katika idara ya misitu Evans Mutari walizuru eneo la chemichemi la Kiu ambapo sherehe ya kitaifa ya upanzi wa miti itaandaliwa na kuanza kuweka mikakati ya kufanikisha zoezi hilo