- 12,213 viewsDuration: 2:06Serikali ya kaunti ya Nairobi imeanza zoezi la kubomoa majumba yote yaliyojengwa kwenye njia za mito. Zoezi hilo limeanzia mtaa wa Westlands baada ya ripoti ya kamati ya mpito ya jiji kuagiza kuwa majumba yote yataathirika na si yale tu yaliyoko kando ya Mto Nairobi. Gavana Johnson Sakaja akisema zoezi hilo linanuia kuzuia athari za mafuriko mara kwa mara jijini.