Kaunti ya Taita Taveta ina idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi

  • | Citizen TV
    346 views

    Kaunti Ya Taita-Taveta ni miongoni mwa kaunti eneo la Pwani ambayo imezidi kushuhudia ongezeko la maambukizi ya virusi vya ukimwi haswa miongoni mwa vijana kati ya umri wa 10-24 , maambukizi mapya ya zaidi ya 659 zikirekodiwa huku jinsia ya kike ikionekana kuathirika zaidi na maambukizi haya ,hii ni kulingana na takwimu za idara ya afya za kitaifa na zile zilizotolewa na idara ya maambukizi ya magonjwa yanayohusikana na ngono kaunti hio. Taita Taveta ikiwa kaunti ya pili katika maambukizi mapya ya virusi hivyo baada ya kaunti ya Mombasa na kwa sasa zaidi ya watu 6,790 wakiishi na virusi hivi ongezeko la asilimia 2.34% katika maambukizi hayo.