KEBS yasema haikuhusishwa kwenye uagizaji wa mbolea

  • | Citizen TV
    126 views

    Mamlaka ya kukadiria ubora wa bidhaa - KEBS - imesema kuwa haikuhusishwa kwenye shughuli nzima ya kuagiza mbolea ambayo sasa inatajwa kuwa ghushi. Aisha mamlaka hiyo inasema kuwa kamati ya kiufundi ndiyo iliyohusika kwenye shughuli hiyo na kebs haikualikwa kukadiria ubora wake. KEBS inasema kuwa ilizuru kampuni ya mbolea ya SBL tarehe 22 mwezi uliopita na kubaini kuwa mbolea iliyokuwepo haikuwa sawa. Ni hapo ambapo KEBS ilibatilisha kibali cha kampuni hiyo na kuiarifu bodi ya Nafaka NCPB kuhusu tahadhari hiyo.