KEG yakashifu serikali kwa kutoa matangazo kwa KBC

  • | Citizen TV
    2,022 views

    Miungano mbalimbali ya wanahabari hii leo imeikashifu serikali kufuatia agizo lake la kufanya matangazo ya kibiashara kupitia shirika la KBC pekee. Akizungumza jijini Nairobi, mwenyekiti wa muungano wa wahariri nchini Zubeidah Kananu amesema kuwa agizo hilo linanuia kukandamiza uhuru wa wanahabari, na kuzima sauti ya wananchi kwa kusababisha mashirika ya habari kukosa mapato. Katika agizo hilo la katibu wa mawasiliano Edward Kisiangani, asasi zote za serikali zinapaswa kutoa kandarasi za matangazo ya kibiashara kupitia shirika la KBC.