Kenya Airways imesitisha mazungumzo na marubani waliogoma

  • | Citizen TV
    3,259 views

    Shirika la ndege la Kenya Airways limesitisha mazungumzo na marubani waliogoma huku likitangaza hasara ya shilingi bilioni moja katika siku tatu ambapo mgomo huo umekuwepo. KQ imesema mgomo wa marubani ni haramu na marubani hawana nia ya kusitisha mgomo. Afisa mkuu wa KQ Allan Kilavuka ametangaza wazi nafasi za kazi za marubani waliogoma akisema 132 kati yao wanajidai kuwa wagonjwa.