Kenya kuandaa kombe la dunia la mchezo roliboli

  • | Citizen TV
    224 views

    Kwa mara ya kwanza, Kenya itakuwa mwenyeji wa mchuano wa dunia wa roliboli kwa chipukizi utakaoanza Jumapili hii katika uwanja wa ndani wa Kasarani. Kenya itakayowakilishwa na vijana chini ya miaka 17 imekuwa kambini kwa wiki moja, kikosi hicho kikiahidi kunyakuwa taji hilo. Mataifa zaidi ya kumi yanayotarajiwa kushiriki mchuano yanaendelea kuwasili nchini. India walikuwa wa kwanza kuwasili ijumaa.