- 15,139 viewsDuration: 1:52Kenya imesema itazungumza na Urusi kuhusu ongezeko la raia wake wanaoajiriwa kupigana katika vita dhidi ya Ukraine, ikikielezea kitendo hicho kama kisichokubalika. Waziri wa mambo ya nje wa taifa hilo Musalia Mudavadi ameiambia BBC kwamba majadiliano yake na serikali ya Moscow yatajikita katika kuhakikisha usalama wa Wakenya na kukabiliana na vitendo vya ajira haramu, ikiwemo majadiliano kuhusu hati za kusafiria na mkataba wa pande mbili unaohusu ajira. Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Peter Mwangangi, Mudavadi amesema mamlaka imefunga takriban mashirika mia sita yaliyokuwa yakiwalaghai Wakenya kwa ajira za ughaibuni. 🎥: @brianmala #bbcswahili #kenya #urusi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw