Kenya na Congo Brazzavile zaafikia kuondoa vikwao vya usafiri

  • | Citizen TV
    605 views

    Kenya na taifa la Jamhuri ya Congo zimeafikiana kuondoa vikwazo vya usafiri kati ya mataifa hayo mawili kama njia moja ya kuimarisha ushirikiano haswa wa kibiashara. Akizungumza baada ya kufanya mkutano na rais wa Congo Denis Sassou N’guesso mjini Brazzaville, Rais Ruto alisema mataifa haya mawili yatashirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo usafiri, utalii na elimu. Hatua ya kwanza Kenya inanuia kuchukua ni kufungua ubalozi wake mjini Brazzaville. Mikataba 18 ya ushirikiano pia ilitiwa saini. Rais Ruto anatarajiwa hapo kesho kuongoza mkutano wa igad kuangazia usalama nchini Sudan.