Kenya na Haiti zatia mkataba wa Kenya-Haiti Nairobi leo

  • | Citizen TV
    2,259 views

    Mpango wa serikali wa kuwatuma maafisa wa polisi elfu moja nchini Haiti umekumbwa na misukosuko kufuatia kuzuka upya kwa mapigano na ghasia katika taifa hilo. Mapigano hayo yalizuka wakati ambapo waziri mkuu wa Haiti Ariel Henri yuko nchini Kenya kutia saini mkataba wa kuharakisha mpango huo. Maelfu ya watu walilazimika kuhama kwao katika mji mkuu wa Port-au-Prince kufuatia ufyatulianaji risasi uliozuka kati ya magenge kadhaa