- 1,954 viewsDuration: 2:43Kenya na Somalia zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kurahisisha usafiri, kufuatia mvutano uliozuka siku ya Jumapili baada ya Kenya kuwazuia baadhi ya maafisa wa Somalia, akiwemo waziri mmoja wa Somalia, kuingia nchini. Hatua hiyo ilizua malalamishi kutoka kwa raia wa Somalia kuhusu ugumu wa kupata viza za usafiri kuingia Kenya. Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia, Abdisaalan Abdi Ali, alikutana na mwenzake wa Kenya Musalia Mudavadi siku ya Jumanne nchini Ethiopia kutafuta suluhisho. Willy Lusige anaarifu zaidi.