Kenya yajiunga na ulimwengu kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani

  • | K24 Video
    32 views

    Huku dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya amani hii leo, nchini kenya tume ya mshikamano wa kitaifa, NCIC imewataka wabunge kupitisha mswada wa mshikamano wa kitaifa na udumishaji amani ambao unaipa tume uwezo wa kukabiliana kisheria na wanaohatarisha amani nchini. Wakati huohuo shirika la haki afrika limetaka kuwepo kwa ushirikiano kati ya maafisa wa usalama na wananchi katika kaunti za Lamu naTana River ili kufanikisha juhudi za usalama katika maeneo hayo.