Kero la kelele : Vilabu Malindi vyafungwa

  • | KBC Video
    48 views

    Watekelezaji wa sheria ya mazingira katika kaunti ya Kilifi wamelivamia vilabu mbali mbali vya burudani vilivyomo katika maeneo ya makazi mjini Malindi kufuatia malalamishi ya wakazi kuhusu kero la kelele.Uvamizi huo unajiri baada ya wasimamizi wa vilabu hivyo kukaidi amri ya kuzingatia kanuni za kelele iliyopiku viwango licha ya kupokea onyo mara kadhaa. Kwa zaidi ya miaka mitatu wakazi hao wakiongozwa na wakili Nikolas Ranford, wamekuwa wakilalama kuhusu kero la kelele kutoka maeneo hayo ya burudani. Watekelezaji wa sheria ya mazingira wamekariri kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wamiliki wa vilabu wanaokaidi amri ya kanuni za kelele

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive