Kesi inayomkabili Maina Njenga yaendelea kusikizwa kwa siku ya pili mtawalia

  • | Citizen TV
    354 views

    Kesi inayomkabili aliyekuwa kiongozi wa kundi la Mungiki Maina Njenga pamoja na washtakiwa wengine kumi na mmoja inaendelea kusikizwa kwa siku ya pili mtawalia. Jana ilikua zamu ya inspekta wa polisi Samson Tanui kutoa ushahidi wake dhidi ya washukiwa hawa wanaokabiliwa na mashtaka 11. Inspekta Tanui alikuwa na wakati mgumu kuelezea mahakama anachojua na kuwahusisha washtakiwa hawa kwenye ushahidi wake alipohojiwa na wakili wa washtakiwa Ndegwa Njiiru. Leo ni zamu ya afisa wa polisi Athumani Asimani kutoa ushahidi wake.