Kifo cha Mwanasiasa Mkongwe Lawrence Sifuna Simiyu

  • | West TV
    234 views
    Aliyekuwa mbunge wa bungoma kusini (sasa kanduyi) lawrence sifuna amefariki. Sifuna ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa bumula alitangazwa kufariki akiwa na umri wa miaka 77. Kwa mujibu wa familia mbunge huyo wa zamani aliugua ugonjwa wa kiharusi(stroke) siku chache zilizopita. Lawrence sifuna alichaguliwa kwa mara ya kwanza kama mbunge mnamo novemba 8, 1979, katika eneo bunge la bungoma kusini wakati huo. Alikitetea tena kiti chake mnamo 1983 . Alishindwa na aliyekuwa kamishna wa mkoa wa kaskazini mashariki maurice makhanu katika uchaguzi mkuu wa 1988 baada ya eneo bunge la bungoma kusini kubadilishwa jina na kuwa kanduyi. Sifuna alitwaa tena kiti hicho wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi wa 1992 kupitia tiketi ya ford asili.