Kijana wa miaka 17 adaiwa kufariki baada ya kupigwa na walinzi wa Kabu ya VVIP RoofTop

  • | Citizen TV
    5,557 views

    Maafisa wa polisi wanaendelea kuwazuilia walinzi wawili wa eneo la burudani la VVIP Rooftop hapa jijini nairobi kutokana na kifo cha kijana wa umri wa miaka 17. Inadaiwa kijana huyo alifariki baada ya kupigwa na walinzi hao ambao waliuficha mwili wake hadi siku iliyofuata huku upasuaji wa maiti ukionyesha kwamba alifariki kutokana na kupigwa kwa muda mrefu.