- 437 viewsDuration: 3:29Wakulima katika baadhi ya maeneo ya Kaunti ya Baringo kwa muda mrefu wamekumbwa na ukame wa mara kwa mara, hali iliyosababisha mifugo kuangamia kutokana na ukosefu wa malisho wakati wa kiangazi. Lakini katika eneo la Molo-Sirwe, Kaunti Ndogo ya Mogotio, kundi la wakulima sasa limebadilisha simulizi hii kwa kugeukia kilimo cha nyasi kavu kama kinga dhidi ya athari za mabadiliko ya hali ya anga.