- 85 viewsDuration: 4:20Kama moja ya njia za kufufua kilimo kilichokuwa kimefifia cha kahawa ya robusta katika kaunti ya Busia, serikali ya kitaifa kupitia wizara ya vyama vya ushirika inaendeleza mpango wa kutoa ufadhili wa miche kwa wakulima Busia. Mpango huo unanuia kuhakikisha kuwa idadi kubwa ya wakulima katika kaunti ya Busia wanapata miche na kurejelea kikamilifu kilimo hicho ambacho kinaaminika kuwa na faida.