Kim aifagilia Russia asema jeshi la Russia na watu wake watashinda dhidi ya 'uadui'

  • | VOA Swahili
    955 views
    Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amemwambia Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatano (Septemba 13) kupitia mkalimani kwamba alikuwa na uhakika jeshi la Russia na watu wake watashinda dhidi ya “uadui,” katika kile alichokieleza ni ubeberu wa Magharibi kwenye vita vya Ukraine. Kabla ya kupendekeza kumuombea afya njema Putin katika hafla, alisema ushindi kwa “Russia yenye nguvu,” na udumu urafiki wa Korea na Russia na afya za wote waliohudhuria, Kim alisema alikuwa na imani Russia itashinda katika kile ambacho Moscow inakiita “ni operesheni maalum ya kijeshi” nchini Ukraine. “Nina imani kubwa kuwa ushujaa wa jeshi la Russia na watu wake utakuwa ni urithi wa utamaduni wa ushindi, utaonyesha ujasiri wa heshima ya hali ya juu na taadhima katika operesheni maalum za kijeshi,” Kim alisema kupitia mkalimani kabla ya kunyanyua glasi ya mvinyo. “Jeshi la Russia na watu wake bila shaka watashinda kwa kishindo katika vita hii tukufu kwa ajili ya kuwaadhibu waovu wakubwa wanaodai ubeberu na kusaidia fikra ya kuvamia wengine,” Kim aliongeza. Mashirika ya Ujasusi ya Magharibi yanashuku kuwa Russia inatafuta kununua silaha na risasi kutoka Korea Kaskazini ili kuzitumia katika vita vyake nchini Ukraine, kitu ambacho pande zote Moscow na Pyongyang wamekanusha. #kimjongun #vladimirputin #voa #voaswahili #russia #koreakaskazini - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.