Kina mama washauriwa kuwanyonyesha wanao kikamilifu

  • | KBC Video
    12 views

    Ni asilimia-60 pekee ya watoto wachanga walio na umri wa chini ya miezi-6 hunyonyeshwa kikamilifu, huku asilimia-60 pekee wakinyonyeshwa saa moja baada ya kuzaliwa. Kulingana na wizara ya afya, hali hiyo imehusishwa na unyanyapaa, ukosefu wa habari kuhusu afya ya akina mama wajawazito na wanaojifungua, dhana za kitamaduni na matumizi ya mbinu mbadala za kunyonyesha watoto wachanga. Akina mama wamehimizwa kuwanyonyesha wanao wachanga kwa muda wa miezi sita mfululizo bila kuwapa chakula kingine na kuendelea kwa miaka miwili na zaidi, baada ya kuanza kuwalisha vyakula vya kawaida.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive