Kinara wa Azimio Raila ashtumu serikali kwa kutopambana na visa vya mauaji Shakahola

  • | K24 Video
    87 views

    Kinara wa Azimio La Umoja Raila Odinga ameishtumu serikali kwa kutopambana na visa vya mauaji ya shakahola kwa wakati uliofaa. Akiikosoa serikali Raila ameitaka serikali ya Kenya Kwanza kuweka wazi uhusiano wake na washukiwa wa mauaji ya Shakahola waliokamatwa. Vile vile ameitaka serikali kuvipa nafasi vyombo vya habari kufika katika eneo hilo ili kuangazia kinachoendelea. Muungano wa Azimio la Umoja umelitaka bunge kuingilia kati suala hilo la maafa Shakahola.