Kinara wa Azimio Raila Odinga amshtumu Francis Atwoli

  • | K24 Video
    382 views

    Kinara wa Azimio Raila Odinga amemshtumu katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU, Francis Atwoli kwa kuwatelekeza wafanyikazi nchini kufuatia hatua yake ya kuunga mkono serikali ya Rais William Ruto. Odinga amemkashifu Atwoli akisema amewasahau wafanyikazi katika wakati anaohitajika zaidi na kumtaka awajibike. Kinara huyo wa upinzani aliyekuwa akihudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa muungano wa vyama vya wafanyikazi COTU Rajab Mwondi katika kaunti ya vihiga pia amemkashifu Rais Ruto kwa matamshi yake anayodai yanatishia mshikamano wa kitaifa.