Kinara wa Azimio Raila Odinga ataka kundi la "Cherera 4' lirudishwe katika tume

  • | K24 Video
    188 views

    Kinara wa Azimio Raila Odinga ametia doa uteuzi wa jopo lililobuniwa kusaili mwenyekiti na makamishna watano wa IEBC. Odinga anadai walioteuliwa ni marafiki wa serikali ambao wanapanga njama za kuhitilafiana na matokeo ya uchaguzi ujao wa urais. Hii leo wanajopo hao saba waliapishwa na jaji mkuu Martha Koome, aliyewaonya kuwa imani ya wakenya ipo mikononi mwao na ni jukumu lao kuhakikisha makamishna watakaoteuliwa ni waaminifu na wenye uwezo wa utendakazi.