Kinara wa DCP apinga hoja ya Raila ya mazungumzo

  • | Citizen TV
    9,789 views

    Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua amepinga mapendekezo ya kuanzishwa kwa mazungumzo mengine ya kitaifa, akisema serikali inafaa tu kutekeleza ripoti za awali za mazungumzo kabla ya kuanzisha mchakato mwingine. Akizungumza alipohudhuria ibada katika jimbo la Seattle nchini Marekani, Gachagua alisema mikakati hiyo ya mazungumzo ni ya kuzima msukumo wa kutaka Rais William Ruto kuondoka mamlakani.