- 348 viewsDuration: 1:41Kinara wa chama cha United Green Movement UGM David Maraga ameisuta serikali kwa kile anasema ni kuendeleza ufisadi kupitia maafisa wake wakuu. Akizungumza mjini Voi kaunti ya Taita Taveta Maraga anasema sakata ya hivi punde ya shilingi bilioni 11 ya uwanja wa Talanta ni ishara tosha serikali haijajitolea katika vita dhidi ya ufisadi. Aidha Maraga akisema wataendelea na ziara za kaunti mbalimbali kuhimiza wananchi kujiandikisha kama wapiga kura.