Kinara wa WIPER Kalonzo Musyoka akosoa ubomoaji unaoendelea Mavoko

  • | Citizen TV
    483 views

    Kinara wa WIPER, Kalonzo Musyoka, amekosoa vikali shughuli ya bomoa bomoa inayoendelea katika eneo la Athi River kaunti ya Machakos akisema kuwa hatua hiyo inakiuka katiba. Akizungumza mjini Bondo, Kalonzo amesikitika kuwa katika bomoa hiyo taasisi za masomo pia hazijasazwa licha ya kuwa watahiniwa wanajiandaa kufanya mitihani ya kitaifa akisema mustakabali wao wa Maisha umeyumbishwa ghafla. Zaidi ya makazi 50 Pamoja na makanisa na misikiti yamebomolewa kuanzia Ijumaa iliyopita kufuatia uamuzi wa mahakama kuu ya Machakos kuwa unyakuzi wa ardhi hiyo ya Kampuni ya Saruji ya East Africa Portland ulikuwa kinyume cha sheria.