Kindiki: Hakuna uhasama serikalini

  • | Citizen TV
    3,715 views

    Naibu wa Rais Kithure Kindiki amepuuzilia mbali tetesi na uvumi wa kuwepo uhasama serikalini na kuwataka wakenya kuzingatia masuala muhimu ya ujenzi wa taifa.

    Akiwahutubia ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria hafla ya harusi kati ya peter miano na wambui kibe katika eneo la Tigoni, kaunti ya Kiambu, Kindiki amesema alikuwa likizoni kwa mapumziko mafupi na amerejea, tayari kwa kibarua cha mwaka huu cha kuboresha uchumi wa nchi na utekelezaji wa miradi ilioasisiwa na utawala wa Rais William Ruto. Bwana harusi ni mwanawe waziri wa utalii Rebecca Miano.