Kiongozi wa Azimio la Umoja Raila asema huenda maandamano yakarejelewa

  • | Citizen TV
    7,413 views

    Kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga amemuonya Rais William Ruto dhidi ya kuweka vikwazo kuhusu mazungumzo baina ya Kenya Kwanza na Azimio. Mazungumzo hayo yakitarajiwa kuanza wiki ijayo, Raila amesema iwapo suluhu ya kutatua masuala waliyoibua haitapatikana, basi wana Azimio watarejelea maandamano. Odinga amepuuzilia mbali madai ya viongozi wa kenya kwanza kuwa lengo la Azimio ni kuingia serikalini kupitia mlango wa nyuma akisema walichotaka ni jamii zilizotengwa na serikali zijumuishwe katika nyadhifa zilizopo.