Kiongozi wa Waislam Atoa Wito wa Kusitishwa Vita Duniani

  • | VOA Swahili
    136 views
    Mwaka huu biashara katika soko la Islee, Nairobi wafanyabiashara wanasema idadi ya mauzo imeshuka. Lakini bado wafanyabiashara wanasema wanaendelea kuingiza bidhaa kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Dubai, Yemen na Uturuki. Mwandishi wa VOA Zeinab Saidi anaeleza kuwa viongozi wa dini wanaeleza kuwa gharama ya maisha imepanda na hivyo kutoa wito kwa serikali ya Kenya kuchukua hatua kupunguza mfumuko wa bei ambao unawaathiri wananchi. Pia Imam wa Msikiti Nairobi anatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kusitisha vita vinavyoendelea duniani hivi sasa, akisisitiza kuwa mafundisho ya Uislam yanataka kile unachopendelea wewe kama ilivyo furaha ya siku ya Eid pia umpendelee ndugu yako na jirani yako. Endelea kusikilza... #waislam #sherehe #sikukuu #iddelfitr #afrikamashariki #sheikh #imam #msikiti #nairobi #gharama #mfumukowabei #bidhaa #dubai #yemen #uturuki