Kisa cha mauaji ya kutatanisha ya ajuza wa miaka 60 huko Kirinyaga

  • | K24 Video
    214 views

    Wakaazi katika mtaa wa Kahiro, wadi ya Mukure , kaunti ya Kirinyaga waliamkia tukio la kushangaza kufuatia kisa cha mauaji yaa ajuza wa miaka 60. Mama huyo anayejulikana kama Esther Wambui Muthike aliuawa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana kisha mwili wake kutupwa katika shamba la kahawa. Haya yanajiri huku mwanaume mwenye umri wa miaka 47 pia kuuawa kwa kukatwa katwa na fahali katika Boma la seneta wa Kakamega Boni Khalwale.