Kitendawili cha utekaji nyara wa Mbunge Koimburi

  • | Citizen TV
    12,609 views

    Mwakilishi wadi wa Kanyenyaini kaunti ya Murang'a Grace Nduta amekamatwa na maafisa wa upelelezi na kuhojiwa kuhusu sakata ya utekaji nyara ya mbunge wa Juja George Koimburi. Nduta anadaiwa kuonana na mbunge huyo wakati ambapo taarifa za kutekwa nyara kwake zilikuwa zikisambaa. Haya yanajiri huku polisi wakidai kuwa koimburi alipanga njama ya kujiteka nyara ili kukwepa mtego wa kumkamata kwa madai ya ulaghai wa ardhi