Kitendawili kuhusu usukaji upya wa tume ya IEBC

  • | K24 Video
    82 views

    Maswali yanazidi kuibuliwa kuhusiana na mustakabali wa wananchi katika maeneo tisa kunakotarajiwa chaguzi ndogo nchini baada ya baadhi ya viongozi kufariki na kwingine uchaguzi kufutiliwa mbali. Kisheria, tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC haiwezi kuandaa chaguzi hizo kwa kukosa idadi kamili baada ya makamishna Abdi Guliye, Boya Molu na mwenyekiti Wafula Chebukati kukamilisha muda wao. Mwabahabari wetu Electine Odera anategua kitendaliwi kilichoko kwa IEBC mwaka huu wa 2024.