Kiungo wa kati wa Real Madrid Eduardo Camavinga apata jeraha

  • | VOA Swahili
    726 views
    Kiungo wa kati wa Real Madrid Eduardo Camavinga alipata jeraha la kwenye goti alipokuwa akifanya mazoezi na timu ya taifa ya Ufaransa, klabu hiyo ilisema Ijumaa. Camavinga, 21, alipata jeraha la goti lake la kulia jumatano alipokuwa akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Ufaransa kwa ajili ya mechi za kufuzu Euro 2024 na kisha kurejea Uhispania kufanyiwa vipimo vilivyoonesha ukubwa wa tatizo hilo. Real haijasema lolote mara moja kama atakaa nje kwa muda gani, lakini majeraha makubwa ya goti huwa yanahitaji miezi kadhaa kupona.