Skip to main content
Skip to main content

Kizaazaa kituoni cha polisi Kapsabet

  • | Citizen TV
    3,445 views
    Duration: 2:32
    Kizaazaa kilizuka katika kituo cha polisi cha Kapsabet Katika kaunti ya Nandi wakati mamia ya wakazi na mwanasiasa mmoja walipovamia kituo hicho wakiwalaumu polisi wanaodaiwa kuharibu gari lake kwa makosa ya trafiki wiki mbili zilizopita. Collins Chepkulei aliyegonga vichwa vya habari kwa kuanzisha kituo cha polisi cha Cheboror katika kaunti ya Uasin Gishu mwaka jana, aliingia kwenye kituo cha polisi cha Kapsabet akiandamana na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wake na kuzua fujo. Akizungumza kwenye kituo hicho alikashifu kitendo cha polisi kuharibu gari akidai alitii amri ya maafisa wa trafiki ila wakatia masikio nta..