Kizaazaa mahakamani Thika

  • | Citizen TV
    5,090 views

    Kizaazaa kilishuhudiwa nje ya mahakama ya Thika baada ya watu 58 walioshtakiwa kwa kuhusika kwenye vurugu na uporaji wakati wa maandamano ya saba saba kuagizwa kulipa dhamana ya shillingi laki moja kila mmoja. Familia zao zilipokea habari hizo kwa mihemko na kutatiza shughuli mahakamani huku zikitishia kuandamana nao hadi wanakozuiliwa.