KNBS : Yadaiwa asilimia 64 ya wafanyakazi ni kutoka jamii-5

  • | KBC Video
    2,182 views

    Kamati ya bunge la seneti kuhusu uwiano wa kitaifa, fursa sawa na mshikamano wa maeneo imeibua wasiwasi kuhusiana na muundo wa wafanyikazi katika shirika la kitaifa la takwimu nchini-KNBS ambapo jamii tano pekee zinajumuisha asilimia-64 ya nafasi za ajira zilizoko. Akiwa mbele ya kamati hiyo, mkurugenzi mkuu wa shirika la KNBS, Dkt Macdonald George Obudho alikuwa na wakati mgumu kuelezea ni kwa nini jamii hizo husika pia zina idadi kubwa ya watu katika mchakato wa uajiri wa hivi punde uliofanywa na shirika hilo, kinyume na miongozo iliyotolewa kwenye katiba ya mwaka-2010 kuhusu fursa sawa za ajira katika taasisi za serikali.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive