K’ogalo watamba FKF Cup

  • | Citizen TV
    667 views

    Klabu ya Gor Mahia imepata ushindi wa moja bila dhidi ya Kibra Soccer katika mechi ya FKF Cup iliyoandaliwa katika uga wa Moi Sports Centre Kasarani. Kocha wa K’ogalo Jonathan Mckintry alipumzisha wachezaji wengi ambao wameshiriki mechi nyingi za ligi. Hata hivyo K’ogalo walipata bao lao katika dakika ya 33 kupitia mchezaji Lloyd Khavichi. Klabu ya Gor Mahia sasa itasubiri kujua ni klabu gani itakayocheza nayo katika raundi ya 16 bora.